Genesis 13:2-6

2 aWakati huo Abramu alikuwa tajiri sana wa mifugo, fedha na dhahabu.

3 bKutoka Negebu, akapita mahali hadi mahali, hadi akafika Betheli, mahali hapo ambapo mwanzoni alipiga hema lake kati ya Betheli na Ai 4 chapo ambapo alikuwa amejenga madhabahu ya kwanza. Huko Abramu akaliitia jina la Bwana.

5 dBasi Loti, ambaye alikuwa anafuatana na Abramu, alikuwa pia na makundi ya mbuzi, kondoo, ngʼombe na mahema. 6 eLakini nchi haikuwatosha kukaa pamoja kwa ajili ya wingi wa mali zao.
Copyright information for SwhNEN